Kanali 14 ya televisheni ya Israel imetangaza kwamba, taarifa za hivi karibuni za Avi Dichter kufutwa kazi mkuu wa zamani wa genge la kijasusi la Israel Shin Bet zinafichua hatari halisi iliyoukumba utawala wa Kizayuni kutokana na kupoteza kuaminiana kati ya waziri mkuu wa Israel na idara za usalama za dola hilo katili.
Kwa mjiujbi wa Dichter, mgogoro wa kutoaminiana umegubika pia uwezo wa kiusalama wa Israel.
Kwa mujibu wa afisa huyo wa zamani wa usalama wa utawala wa Kizayuni, kutoaminiana huko kunaweza hata kuathiri usalama binafsi wa Benjamin Netanyahu, kwani kutoaminiana huko kunadhoofisha pia uwezo wa Shin Bet wa kutekeleza operesheni zake.
Mkurugenzi huyo wa zamani wa genge la kijasusi la Shin Bet la Israel ameongeza kuwa, kukosekana kuaminiana kunasababisha pia hatari za kila siku kwa madhara ya waziri mkuu kwani kumepelekea muundo wa usalama kwa ujumla kukumbwa na mgogoro na hatari, na kwa sababu hiyo, uwezo na nguvu za kitaasisi za kukabiliana na vitisho vya nje na vya ndani zimedhoofika.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, ilifichuka kuwa washauri wawili muhimu wa waziri mkuu wa Israel Benjami Netanyahu wanachunguzwa kwa kupokea pesa nyingi kutoka Qatar na hazijulikani ziliishia wapi. Uchunguzi huo unakaribia hatua zake za mwisho suala ambalo limemkasirisha Netanyahu na kuamua kumfuta kazi mkuu wa genge la kijasusi la Israel, Shin Bet linalofanya uchunguzi huo.
342/
Your Comment