24 Machi 2025 - 18:15
Source: Parstoday
Pezeshkian: Marekani haiwezi kulikwamisha taifa la Iran katika jambo lolote

Rais Masoud Pezeshkian amesema kwamba Marekani haiwezi kuiwamisha Iran katika jambo lake lolote lile iwapo taifa hili la Kiislamu litashikamana vilivyo na mafundisho ya Qur'ani na ya Uislamu.

Rais Pezeshkian amesema hayo kwenye hotuba fupi aliyoitoa katika mkesha wa Laylatul Qadr wa kuamkia leo Jumatatu mwezi 23 Ramadhani 1446 Hijria katika Chuo Kikuu cha Tabriz na kuongeza kuwa, kila kitu kinachotakiwa na taifa la Iran kinapatikana kwenye Qur'ani Tukufu na mafundisho ya Bwana Mtume Muhammad SAW na Ahlul Bayt wake AS na kwamba adui hawezi kulizuia taifa hili kufikia malengo yake.

Mkesha huo wa Laylatul Qadr umefanyika kwenye Msikiti wa Rasulullah katika Chuo Kikuu cha Tabriz na Rais ameshiriki kwenye mkesha huo bila ya maandalizi na hatua kubwa za kiusalama na kukaa chini pembeni mwa Waislamu wengine.

Katika hotuba hiyo fupi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kila tulicho nacho kinatokana na Qur'ani na Ahlul Bayt (AS). Qurani ni Kitabu kilichoteremshwa kwa watu katika usiku wenye cheo wa Laylatul Qadr ili kiweze kufanyiwa kazi. Ikiwa tutakuwa tunakisoma tu Kitabu hiki kitukufu bila ya kutendea kazi maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyomo ndani yake, tutakuwa kama watu wanaobeba tu vitabu bila ya kujua thamani zake.

Rais Pezeshkian amesema, Kuifanyia kazi Qur'ani Tukufu kunapaswa kuwe na athari katika maisha yetu; kunapaswa kutuongoza kwenye nuru kutoka kwenye giza na kutoka kwenye unyonge kwenda kwenye nguvu na heshima.

Hapa chini tumeweka picha chache zinazoonesha wakati Rais Pezeshkian aliposhiriki kwenye mkesha huo wa Laylatul Qadr jana usiku.

Pezeshkian: Marekani haiwezi kulikwamisha taifa la Iran katika jambo lolotePezeshkian: Marekani haiwezi kulikwamisha taifa la Iran katika jambo lolotePezeshkian: Marekani haiwezi kulikwamisha taifa la Iran katika jambo lolote

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha