24 Machi 2025 - 18:16
Source: Parstoday
Iran: Tuko imara! Hakuna mtu anayeweza hata kufikiria kuanzisha vita dhidi yetu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Majeshi na serikali yetu tumeijengea nchi kinga ya kutosha kiasi kwamba hakuna hata mtu anayeweza kufikiria kuanzisha vita dhidi ya Iran."

Sayyid Abbas Araqchi amesema hayo kwa kujiamini wakati alipotembelea makao makuu ya Kamati ya Nairuzi ya Jumuiya ya Hilali Nyekundu na kusema: "Vikosi vya ulinzi na serikali (ya Iran) vimejitayarisha kwa hali yoyote ile, na vikosi vya kutoa misaada pia vimejitayarisha vilivyo. Na hii inajenga kinga kwa nchi, kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kufikiria kuanzisha vita dhidi ya Iran."

Amesema: "Maandalizi yetu haya yanajenga kinga kwetu na kutufanya tuweko tayari kikamilifu kwa hali yoyote ile."

Kabla ya hapo pia yaani juzi Jumamosi, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Kiumars Heidari alikuwa amesema kwamba kikosi chake kiko macho na tayari kabisa kuwaangamiza maadui endapo watathubutu kufanya makosa yoyote dhidi ya taifa kubwa la Iran.

Amesema: "Kikosi cha Nchi Kabu cha Jeshi la Iran daima kiko macho, ange na tayari kusambaratisha maisha ya fedheha ya maadui iwapo kutatokea makosa yoyote." 

Iran: Tuko imara! Hakuna mtu anayeweza hata kufikiria kuanzisha vita dhidi yetu

Brigedia Jenerali Heidari amebainisha kuwa, "Ni muhimu kwa vikosi vya kijeshi vya Iran daima kuimarisha utayari wao wa vita na uwezo wa kuzuia hujuma, ili kudhamini usalama endelevu wa Jamhuri ya Kiislamu."

Kamanda huyo mwandamizi wa Iran amebainisha, kuwa Vikosi vya Nchi Kavu vinajaribu kudumisha umakini wao kamili na kutegemea mafanikio ya hali ya juu ya ulinzi na usalama ili kudumisha usalama wa mpaka.

Matamshi hayo ya viongozi wa Iran yametolewa wakati huu ambapo rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kupiga ngoma ya vita dhidi ya Iran, huku akidai kuwa Tehran inaweza kukabiliwa kwa chaguo la kijeshi iwapo hakutafikiwa makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Kamanda Heidari ameeleza kuwa, "Kinachowatia kiwewe maadui wa Jamhuri ya Kiislamu hata zaidi ya silaha za kijeshi, ni taifa kubwa la Iran na uungaji mkono wa wananchi kwa mfumo wao wa utawala."

Iran inasema, inajibu vitisho vya maneno vya adui kwa vitisho na iwapo adui atafanya kosa la kutekeleza kivitendo vitisho vyake, basi majibu ya kivitendo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatakuwa makali mno.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha