24 Machi 2025 - 18:19
Source: Parstoday
Siku ya saba ya uvamizi wa Israel wa Ghaza; makumi wauawa na kujeruhiwa

Utawala wa wa Kizayuni wa Israel Israel unaendelea kufanya jinai na mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza ambapo tangu asubuhi ya leo hadi wakati tunaandaa taarifa hii, makumi ya Wapalestina wamekuwa wameshauwa shahidi na kujeruhiwa, leo ikiwa ni siku ya saba ya tangu kuanza wimbi jipya la jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

Mapema leo asubuhi na katika taarifa zake za sekunde kwa sekundi, televisheni ya Al Jazeera ilitangaza kwamba, Wapalestina 21 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya anga ya Israel katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza ya leo asubuhi na makumi ya wengine wamejeruhiwa.

Duru za Palestina zimetangaza kuwa: Mashambulio ya anga ya jeshi katili la Israel leo yameanza tena katika miji miwili ya Khan Yunis na Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza.

Duru mbalimbali za habari zimetangaza kuwa, katika taarifa za awali za mashambulizi ya leo asubuhi ya Israel, Wapalestina wasiopungua 15 wameuawa shahidi wakati utawala wa Kizayuni uliposhambulia mahema yao huko Qayzan Rashwan kusini mwa Khan Yunis.

Katika wimbi hili jipya la mashambulizi ya kikatili ya Israel, viongozi mbalimbali wa makundi ya Muqawama hasa HAMAS na Jihadul Islami nao wameuawa shahidi ikiwa ni kuthibitisha kwamba viongozi wanamapambano wa Palestina ni sehemu ya jamii na yanawafika yaleyale yanayowafika wananchi wengine wa Palestina.

Kituo cha kibiashara katika mji wa Al-Zawaida katikati mwa Ukanda wa Ghaza pia kililengwa na mashambulizi ya anga ya jeshi katili la Israel. Watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio la anga la Wazayuni kwenye hema la Mohib ambalo ni makazi ya wakimbizi katika eneo la Al-Swarah katikati mwa ukanda wa Ghaza.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha