24 Machi 2025 - 21:41
Source: Parstoday
Mawakili 77 wa Ujerumani waitaka serikali iheshimu hukumu ya ICC ya kumkamata Netanyahu

Mawakili 77 mashuhuri wa Ujerumani wametoa tamko la kuunga mkono uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kuagiza waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe na kuitaka serikali ya shirikisho ya Ujerumani iheshimu uamuzi huo.

Katika taarifa yao ya pamoja, mawakili hao wameitaka serikali ya shirikisho ya Ujerumani iheshimu sheria za kimataifa kuhusiana na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai wa kuagiza waziri mkuu wa Israel akamatwe na kufikishwa mbele ya mahakama hiyo.

Wanasheria hao wameeleza pia kwamba, endapo Netanyahu ataruhusiwa kuingia Ujerumani, hatua hiyo itakuwa ni ukiukaji wa haki na sheria zinazotawala nchi hiyo.Aidha, taarifa ya wanasheria hao imekosoa hatua ya baadhi ya vyuo vikuu vya Ujerumani ya kufuta mhadhara uliopangwa kutolewa na Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Francesca Albanese.

Afisa maalumu wa serikali ya shirikisho ya Ujerumani anayehusika na "kupambana na chuki dhidi ya Uyahudi" alidai hivi karibuni kuwa hotuba za ripota huyo maalumu wa UN zina "maelezo ya chuki dhidi ya Uyahudi".Friedrich Mertz, Kansela ajaye wa Ujerumani, alitangaza wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba, atapata njia na nyenzo zinazohitajika ili kumwezesha Netanyahu kuingia nchini Ujerumani.

Katika usiku wa uchaguzi na baada ya kutangazwa mshindi, Meretz alifanya mazungumzo ya simu na waziri mkuu huyo wa utawala wa Kizayuni anayetakiwa akamatwe na kukabidhiwa kwa Mahakama ya ICC.

Mwezi Novemba 2024, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yenye makao yake The Hague, Uholanzi ilitoa waranti wa kukamatwa Netanyahu na aliyekuwa waziri wa vita wa Israel Yoav Gallant kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu, na kutumia njaa (kwa kuwaweka na njaa watu wa Gaza) kama silaha.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha