Magnier ameeleza hayo katika mahojiano na televisheni ya Aljazeera na kubainisha kuwa Netanyahu "anafanya hivyo na Syria, bila ya kuchokozwa na Syria; anafanya hivyo pia na Lebanon".
Kwa mujibu wa mchambuzi huyo wa masuala ya kijeshi wa Brussels, Ubelgiji, madai ya utawala wa Kizayuni kwamba siku ya Jumamosi ulishambuliwa kwa makombora matano yaliyotokea Lebanon "yanatia shaka", akisema si jambo "lenye thamani" kwa Hizbullah au makundi mengine yanayobeba silaha kutekeleza shambulio kama hilo, jambo ambalo limethibitishwa na mashambulio ya 'kujibu' yapatayo 200 yaliyofanywa na jeshi la Israel ambayo yameua watu saba na kujeruhi wengine kadhaa nchini Lebanon.
Magnier amebainisha kuwa ni muhiumu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuendeleza mashinikizo hayo ya kijeshi kwa sababu za kisiasa na kumnufaisha pia kisiasa Netanyahu na baraza lake la mawaziri la mrengo wakulia wenye misimamo ya kufurutu mpaka.
Siku ya Jumamosi, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah ilitoa taarifa ya kukanusha kuhusika kwa namna yoyote na shambulio la maroketi lililodaiwa na utawala wa Kizayuni kwamba limefanywa kutokea Lebanon na kulenga maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina bandia la Israel.
Taarifa ya Hizbullah ilieleza bayana kwamba, madai ya adui Mzayuni yanalenga kuhalalisha mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya Lebanon ambayo hayajasita tangu yalipotangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati yake na harakati hiyo ya Muqawama wa Lebanon.../
342/
Your Comment