-
70 wauawa katika mapigano baina ya pande kinzani Syria
Zaidi ya watu 70 wameripotiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Syria kutokana na mapigano makali kati ya wanamgambo wa kundi la kigaidi linalotawala la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) na makundi ya Muqawama ya wananchi huko magharibi mwa nchi hiyo.
-
Askari wa Israel wavamia misikiti mjini Nablus na kuzuia Swala ya Ijumaa
Vikosi vya jeshi la Israel vimevamia misikiti kadhaa katika mji mkongwe wa Nablus, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kuzuia kuswaliwa Swala ya Ijumaa.
-
India: BRICS haina msimamo wa pamoja kuhusu suala la kuachana na sarafu ya dola ya Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar amesema, dhana ya kwamba kundi la mataifa ya BRICS linafanya juu chini kukabiliana na sarafu ya dola ya Marekani "haijathibitishwa na ukweli" na akaongeza kuwa, India hasa kwa upande wake "haina nia hata kidogo ya kuidhoofisha sarafu hiyo.
-
Yemen: US kuiweka Ansarullah katika orodha ya ugaidi haina uhalali wowote
Afisa mmoja mwandamizi wa Yemen amepuuzilia mbali hatua ya Marekani ya kuitambua Harakati ya Muqawama ya Ansarullah kama kundi la kigaidi, akisema uamuzi huo hauna uhalali wowote.
-
HAMAS yasema imejiandaa 'kwa chochote kitachotokea' baada ya 'onyo la mwisho' alilotoa Trump
Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kwamba, zimejiandaa kwa "chochote kitachotokea" na zingali ziko kwenye hali ya "tahadhari kamili", zikisisitiza kuwa, vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuanzisha tena vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza havitatoa hakikisho kwa utawala huo dhalimu la kuweza kuwakomboa mateka wake.
-
Mkutano wa viongozi wa Arab League wapasisha mpango wa Misri wa kuijenga upya Gaza
Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) umepasisha mpango wa Misri wa kuijenga upya Gaza na kutaka kutumwa wanajeshi wa kulinda amani katika eneo hilo.
-
Hamas: Kufunga vivuko vya Ukanda wa Gaza ni jinai ya kivita
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesina HAMAS imelaani kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kufunga kwa siku tatu mfululizo vivuko vya Ukanda wa Gaza na kuitaja hatua hiyo kuwa inashadidisha kukiukwa makubaliano ya kusitisha mapigano na ni jinai ya kivita.
-
Mpango wa Umoja wa Nchi za Kiarabu kuhusu Palestina unapingana na matakwa ya Marekani na Utawala wa Kizayuni
Viongozi wa nchi za Kiarabu, katika mkutano wao mjini Cairo, wamepinga mipango na njama za kishetani za Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kukataa hatua za kulazimisha uhamishaji wa Wapalestina.
-
Yemen yaangusha ndege ya 15 ya kisasa ya kijasusi ya Marekani
Jeshi la Yemen limetangaza kuangusha kwa mafanikio ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper baada ya kuingia katika anga ya nchi hiyo kinyume cha sheria na kufanya operesheni za kijeshi katika mkoa wa magharibi wa al-Hudaydah.