Tangu mwaka 2015, Mahakama Kuu ya serikali kuu ya Marekani ilitoa hakikisho la kutambuliwa ndoa za watu wa jinsia moja. Lakini baada ya mahakama hiyo kubadilisha ghafla mtazamo yake juu ya uavyaji mimba, ulizuka wasiwasi mkubwa kwa watetezi wa maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsi moja kwamba haki hiyo pia itapotea.Katikati ya Julai mwaka huu, Baraza la Wawakilishi la Marekani lilipitisha sheria ya kuunga mkono ndoa za jinsia moja nchini kote, ambapo wawakilishi wote wa chama cha Democrat na 47 wa Republican waliunga mkono hati ya sheria hiyo. Hata hivyo wawakilishi wapatao 160 wa Republican walipinga uamuzi huo.Tokea wiki chache zilizopita, mashauriano yamekuwa yakiendelea ndani ya baraza la Seneti kuhakikisha unapatikana uungaji mkono wa angalau maseneta kumi wa chama cha Republican kwa hati ya sheria hiyo, ambao unahitajika ili kuweza kuidhinishwa.
342/