Main Title

source : Parstoday
Jumatano

5 Julai 2023

17:59:30
1377420

Umoja wa Mataifa: Kuna zaidi ya wahajiri wa ndani milioni 71 duniani

Umoja wa Mataiifa umetangaza kuwa, kuna wahajiri wa ndani zaidi ya milioni 71 katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa, wahajiri hao wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na sababu mbalimbalii kama mabadiliko ya tabianchi, machafuko na vita.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kuendelea vita vya Ukraine na kushadidi ukosefu wa amani katika mataifa mbalimbali ya Kiafrika kutokana na harakati za makundi ya kigaidi sambamba na ukosefu wa usalama wa chakula uliosababishwa na majanga ya kimaumbile kama ukame na kadhalika, ni mambo ambayo yamechangia pakubwa kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi duniani.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu idadi kubwa na isiyo na kifani ya wakimbizi katika ripoti ambayo imepewa anwani ya "Mashtaka Dhidi ya Hali ya Sasa ya Dunia." 

Katika mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya hivi sasa nchini Sudan, familia nyingi zimelazimika kuacha nyumba na makazi yao, jambo ambalo lilikuwa tayari limesababisha matatizo makubwa kutokana na vita kati ya Russia na Ukraine, pamoja na hali ya Afghanistan.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe, uvamizi wa madola ya kigeni, matatizo ya kiuchumi kama vile mfumuko wa bei na njaa, matatizo yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama ukame, mafuriko na kadhalika, pamoja na kutafuta maisha bora, ni miongoni mwa sababu kuu zinazowafanya watu wakimbie na kuhama makazi na nchi zao za asili. 

342/