Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

14 Julai 2023

09:58:56
1379299

Balozi wa Iran nchini Kenya: Jamhuri ya Kiislamu imefanikiwa kupanua ushirikiano na nchi za Afrika

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya amesema kuwa utendaji wa Serikali ya Awamu ya 13 umekuwa na mafanikio katika kupanua ushirikiano na Kenya.

Ja'far Barmaki ameyasema hayo baada ya Rais Ebrahim Raisi kukamilisha safari yake katika nchi tatu za Afrika ambazo ni Kenya, uganda na Zimbabwe. Safari hiyo ililenga kustawisha zaidi uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni baina ya Iran na nchi za Afrika. 

Balozi Ja'far Barmaki, ambaye alikuwa akizungumzia mafanikio ya kidiplomasia ya Iran katika nchi za Afrika amesema kuhusiana na malengo na umuhimu wa ziara ya Rais Ebrahim Raisi katika nchi hizo tatu za Afrika kuwa: "Nchi za Afrika zina uwezo mkubwa, na kustawisha uhusiano na nchi hizo kunaweza kudhamini maslahi ya taifa la Iran na mataifa hayo."

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya amesema: Bidhaa za Iran zinaweza kuingia kwa urahisi katika soko la nchi za Kiafrika kwa sababu zina bei nzuri na ubora unaohitajika.

Amesisitiza kuwa; Iran inapaswa kugeukie masoko mapya na kwamba Afrika ni mojawapo ya masoko hayo.

Rasi Ebrahim Raisi amerejea mapema leo nchini baada ya kukamilisha safari yake katika nchi tatu za Afrika. Hiyo ilikuwa safari ya kwanza ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi za Afrika baada ya kipindi cha miaka 11.Akielezea mafanikio ya safari yake baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mehrabad, Sayyid Ebrahim Raisi amesema lengo la safari ya Afrika ni kuimarisha stratijia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika bara hilo na kuongeza kuwa: Uhusiano wa Iran na bara la Afrika, kama ilivyo mahusiano ya nchi hii na nchi za Asia na maeneo mengine ya dunia, una umuhimu mkubwa na fursa ya hiyo haipaswi kupuuzwa.

342/