Kwa mujibu wa Shirika la habari la IRNA, Bahareh Arabi, Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Hali ya Hewa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Mostafavi Darani, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kistratijia ya Idara Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa la mkoa wa Isfahan ameteuliwa kuwa mjumbe mkuu wa "Timu ya Wataalamu kuhusu Ukame" na "Yashar Falamarzi, mjumbe wa Jopo la Masuala ya Elimu la Taasisi ya Utafiti wa Hali ya Hewa na Sayansi ya Anga ya Iran, kuwa mjumbe mshiriki wa "Kamati ya Kudumu ya Huduma za Kihaidrolojia" ambayo iko chini ya usimamizi wa Kamisheni ya Stratijia na Huduma za Hali ya Hewa, Mazingira, Haidrolojia na Bahari" ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani. Wote wawili watahudumu katika nafasi hizo kwa muda wa miaka minne.
Bahareh Arabi Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Hali ya Hewa la Iran ameongeza kuwa haya ni mafanikio ya 14 ya kimataifa ya shirika hilo katika kupata viti vya kimataifa.
Bahareh Arabi amesema viti hivi vimepatiwa wawakilishi wa Iran baada ya kupita miaka isiyopungua 15.
342/