Main Title

source : Parstoday
Jumatano

24 Julai 2024

19:14:20
1474302

Katika barua kwa kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, vijana wa Ubelgiji: Tumefurahishwa sana na ujumbe wako

Katika barua yao kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, idadi kubwa ya vijana wa Ubelgiji wamemshukuru Ayatullah Ali Khamenei kwa barua yake ya hivi karibuni ya kuunga mkono maandamano ya kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza katika vyuo vikuu vya Marekani na Ulaya na kutangaza kwamba, wameathiriwa sana na ujumbe na wito wake.

Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hivi karibuni aliwaandikia barua wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani na Ulaya wanaowaunga mkono na kuwatetea wananchi wa Palestina ambapo mbali na kueleza mshikamano wake na maandamano ya wanafunzi hao dhidi ya Uzayuni, aliwataja wanafunzi hao kuwa ni sehemu ya kambi ya Muqawama na mapambano. Ayatullah Khamenei aliwaambia wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani na Ulaya kwamba: "Mumesimama upande sahihi wa historia" na kuwasihi watalii na kuisoma Qur'ani Tukufu.Katika kujibu barua hiyo, wanafunzi wa vyuo vikuu vya Ubelgiji ameshukuru kwa dhati nasaha za Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu za kuwataka waendelee kuwatetea na kuonyesha mshikamano na watu wa Ukanda wa Gaza na kuandika kuwa:  Vijana wa Ubelgiji wameathiriwa sana na ujumbe wa wito wa kutetea haki na kutafuta ukweli, na vilevile kushikamana barabara na malengo ya kupigania ukombozi ya Wapalestina na watu wanaodhulumiwa kote duniani.

Sehemu moja ya barua ya vijana wa Ubelgiji kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imeeleza kuwa: Juhudi zako zisizochoka za kuhimiza maelewano, uadilifu na mshikamano katika kukabiliana na changamoto tata zina umuhimu mkubwa, na sote tumeazimia kuimarisha uelewa wetu kuhusu Uislamu.

Vilevile, barua hiyo imesema, harakati ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Ulaya na Marekani ya kuiunga mkono Palestina inaonyesha kuwa, vijana wa Kimagharibi wamepata uelewa kuhusu dhulma zinazotendeka duniani. Wamesisitiza pia kuwa wanatazamia kuendelea kwa mabadilishano hayo yenye matunda ya moyo wa mazungumzo na ushirikiano wenye kujenga.

Barua hii imechapishwa katika lugha za Kiajemi, Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu kwa hashtagi ya LETTER4LEADER.


342/