Wengi wanaitathmini hatua hiyo kama mfano wa wazi wa kutoguswa serikali na matatizo ya wananchi wa Nigeria hususan mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaoisumbua nchi hiyo.
Raia mmoja wa Nigeria amesikika akisema kuwa, serikali inatutaka tufunge mikanda huku Rais wa nchi akiruka kwenye ndege mpya. Raia mwingine amesema: "Ununuzi wa ndege hii mpya unaonyesha ni jinsi gani Rais asivyojali masaibu na tabu za watu wa Nigeria."
Oby Ezekwesili, waziri wa zamani wa elimu wa Nigeria amekosoa kununuliwa ndege mpya ya Rais na kukitaja kitendo hicho kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Hata hivyo Msemaji wa Rais wa Nigeria ametetea umauzi huo na kudai kuwa ndege hiyo imenunuliwa kwa bei nafuu kwa ushauri wa Kamati ya Usalama ya Seneti.
342/