23 Aprili 2017 - 20:22
 Kadhi wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah ameritadi kuwa mkristo+ picha

Kadhi wa masuala ya kisheria wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusra aliyekuwa amejiunga na kikundi hicho mwaka 2003 nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kadhi wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusra amebadili dini na kuwa mkristo kwa kubatizwa katika moja ya makanisa ya Ujerumani
“Hasam Abu Hamzah” ambaye alikuwa kadhi na kamanda wa kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah, ambapo alijiunga na kikundi hicho mnamo mwaka 2003, naye alikitumikia kikundi hicho cha kigaidi katika kufanya jinai mbalimbali nchini Iraq na Syria.
Katika maeneo wanayoishi wafuasi wa dini ya Kikristo nchini Syria kiliingia kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah na kuwauwa na kuwachinja kinyama wafuasi wa dini hiyo waliokuwa wanaishi katika sehemu hizo.
Kikundi cha kigaidi cha Jabhatun Nusrah daima kilikuwa kinasisitiza kuwa wafuasi wa dini ya Kikristo ni washirikina na ni jambo la wajibu kuwauwa na kuzisambaratisha mali zao.
Hasam Abu Hamzah alifika katika sherehe za kubatizwa kwake na baada ya kubatizwa alichagua jina la “Paulo” kuwa ndio jina lake, ambapo katika picha alizokuwa amepigwa, pembeni mwa gaidi huyo anaoneka Dokta “Muhammad Rahumah” aliyekuwa msimamizi wa kitivo cha uhakiki wa mambo ya kiarabu katika chuo kikuu cha Minya nchini Misri, ambaye miaka kadhaa iliopita alidai kuwa amekuwa Mkristo na kuamia nchi za Ulaya.
Gaidi huyo ameashiria na kudai kuwa hapo kabla alikuwa anaamini kuwa dini ya kikristo, ilifanya mauaji makubwa sehemu mbalimbali duniani chini serikali ya Marekani, kwa maana nilikuwa naamini kuwa serikali ya Marekani inatekeleza na kufuata mafunzo ya Nabii Isa (a.s), kwani nilikuwa sijahi hata siku moja kitabu cha Injili.

mwisho/290