Main Title

source : Pars Today
Jumatatu

1 Julai 2019

02:24:59
956451

Kwa nini Imarati imeamua kupunguza idadi ya wanajeshi wake huko Yemen?

Baadhi ya duru za habari zimeripoti kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umepunguza idadi ya askari wake waliokuwa katika mji wa Aden huko kusini mwa Yemen.

(ABNA24.com) Baadhi ya duru za habari zimeripoti kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umepunguza idadi ya askari wake waliokuwa katika mji wa Aden huko kusini mwa Yemen.

Imarati na Saudi Arabia ni washirika wakuu katika muungano wa vita dhidi ya taifa madhlumu la Yemen. Imarati imeingilia kisiasa na kijeshi katika kadhia ya Yemen na inashiriki vilivyo katika vita vinavyoendelea kuua raia wasio na hatia nchini humo. Katika upande wa kisiasa pia Imarati imejizatiti katika maeneo ya kusini mwa Yemen na imeteka na kuyakalia kwa mabavu baadhi ya maeneo hayo. Abu Dhabi pia inashindana na mshirika wake, yaani Saudia kwa ajili ya kuwa na satua na ushawishi mkubwa zaidi katika maeneo hayo. 

Hata hivyo serikali ya Imarati inahitilafiana sana na rais aliyejiuzulu na kutorokea Saudi Arabia wa Yemen, Abdrabbuh Mansur Hadi ambaye anaungwa mkono na kusaidiwa na watawala wa Riyadh. Hapa linajitokeza swali muhimu kwamba, ni kwa nini Abu Dhabi imechukua uamuzi wa kupunguza wamajeshi wake katika vita vya Yemen? 

Sababu ya kwana kabisa inahusiana na harakati mpya na hujuma za jeshi na wapiganaji wa kujitolea wa Yemen. Jeshi na wapiganaji hao wa makundi ya kujitolea ya wananchi, katika miezi ya hivi karibuni yametumia uwezo wao wa makombora na ndege zisizo na rubani na kushambulia maeneo muhimu na ya kistratijia ya Saudi Arabia na Imarati. Harakati hii imeonesha udhaifu wa Imarati na kuzusha hitilafu za ndani hususan baina ya mrithi wa kiti cha kiongozi wa Abu Dhabi na mtawala wa Dubai. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, uchumi wa Imarati unategemea biashara, na hali ya ukosefu wa amani wa aina yoyote ni sawa na sumu angamizi kwa nchi hiyo. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Kiarabu Adnan Hasim anasema: "Maamuzi binafsi ya mrithi wa kiti cha mtawala wa Abu Dhabi, Mohammed bin Zayed Al Nahyan katika siasa za nje imezusha hitilafu baina yake na mtawala wa Dubai, Sheikh Muhammad bin Rashid ambaye amekuwa akikosoa taathira mbaya za maamuzi ya Bin Zayed katika siasa za nje kwa uchumi wa Imarati". 

Sababu ya pili inahusiana na mivutano iliyopo baina ya Iran na Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi. Serikali ya Abu Dhabi ambayo ina mchango mkubwa katika kuongezeka mivutano hiyo na hata baadhi ya taarifa za kiintelijensia zinazema kuwa, Imarati ilihusika na shambulizi la tarehe 13 Juni lililolenga meli mbili za mafuta katika Bahari ya Oman, imepatwa na wasiwasi kuhusiana na uwezo mkubwa wa jeshi la Iran juu ya usalama wake hususan baada ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu kutungua ndege ya ujasusi isiyo na rubani ya Marekani.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Yemen, Yasin al Tamimi anasema: "Uamuzi wa Imarati wa kupunguza idadi ya askari wake huko Aden una mfungamano na wasiwasi wa nchi hiyo kuhusu uwezekano wa kuingia katika mivutano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Duru za kidiplomasia pia zimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba kutokana na mivutano iliyopo hivi sasa katika eneo la Ghuba ya Uajemi, Imarati imeona bora kuliondoa jeshi lake huko Yemen na kujiweka tayari. 

Jambo jingine linalopaswa kuashiriwa hapa ni kuwa, kupunguzwa idadi ya askari wa Imarati huko Aden hakuna maana ya kusitishwa ushiriki wa nchi hiyo katika vita vya Yemen, bali katika kipindi cha sasa, viongozi wa Imarati wanaonelea bora kutumia mamluki wa kigeni kama wale wanaotoka Sudan na vibaraka wao wa ndani ya Yemen kwenye kwa ajili ya kutimiza malengo yao nchini humo.   




/129