Main Title

source : Pars Today
Jumapili

14 Julai 2019

08:59:19
960861

China yapinga tena vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China kwa mara nyingine tena amesema kuwa Beijing inapinga vikwazo visivyo vya kisheria na vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran.

(ABNA24.com) Geng Shuang ambaye alikuwa akijibu tahadhari iliyotolewa na Marekani kwamba itaiwekea vikwazo China au nchi nyingine yoyote itakayonunua mafuta kutoka Iran, amewaambia waandishi habari kwamba: "Miamala ya kibishara ya China na Jamhuri ya Kiislamu inafanyika katika misingi ya sheria za kimataifa na kimantiki na Beijing haitasalimu amri mbele ya maamuzi yasiyokuwa ya kisheria ya Marekanii." Shuang ameongeza kuwa uhusiano wa kibiashara wa China na jamii ya kimataifa ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unazingatia sheria za kimataifa na unapaswa kuheshimiwa. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesisitiza kwamba, Beijing inapinga vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran na kuongeza kwamba, China itatetea haki na maslahi yake ya kisheria.  

Hii si mara ya kwanza kwa serikali ya China kutetea ushirikiano wake wa kiuchumi na kununua mafuta ya Iran baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuzidisha vikwazo vyake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Viongozi wa China daima wamekuwa wakisisitiza kwamba wataendeleza ushirikiano wa kiuchumi wa nchi hiyo na Iran kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa hilo na kudhamini mahitaji yao na nishati na kwamba hawaogopi vitisho na mashinikizo ya ikulu ya Rais wa Marekani, White House. 

Msimamo huo mpya wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China wa kuendelea kununua mafuta kutoka Iran unaonesha kuwa, Beijing ambayo ndiye mnunuzi mkubwa zaidi wa mafuta ya Iran na miongoni mwa nchi zilizotia saini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, inapinga vikali sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za Marekani dhidi ya Iran.

Serikali ya Marekani inatumia mabavu na ubabe wa kutaka kuzitwisha nchi nyingine maamuzi na sheria zake za ndani na hapana shaka kuwa mashinikizo ya Washington dhidi ya washirika wakubwa wa kiuchumi wa Iran ikiwemo China na kuwataka wafuate sheria za ndani za Marekani kuhusiana na Iran ni sehemu ya sera hizo za kimabavu. John Dricsole ambaye ni mtaalamu wa masoko ya nishati anasema: "China haijali vitisho vya Marekani, na Beijing pamoja na India ni miongoni mwa waagizaji wakubwa zaidi wa mafuta ya Iran na zinayaona maslahi yao kuwa yamo katika kudumisha ushirikiano wao wa kiuchumi na Tehran. Nchi hizo mbili hazijali kabisa matamshi na vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani."

Mbali na China ambayo imesimama kidete kupinga matakwa yasiyo ya kimantiki na ya kimabavu ya Marekani ya kusimamisha ununuzi wa mafuta kutoka Iran, wanunuaji wengine wakubwa wa mafuta ya Iran wanaopinga matakwa hayo ya Marekani nchi nchi kama India, Korea Kusini na Japan mbazo zinatambua matakwa hayo ya serikali ya Washington kuwa yanapingana na maslahi yao na sheria za kimataifa. Si hayo tu bali hata baadhi ya makumpuni ya China yamesimamisha ununuzi wa mafuta kutoka Marekani na kuanza kununua mafuta ya Iran.

Mtaalamu wa masoko ya nishati Victor Shom anasema: "China ambayo inastawi kwa kasi kubwa sana ina hamu kubwa sana ya kununua mafuta na haiwezi kufumbia macho mafuta ya Iran na maslahi yake."

Kwa kutilia maanani haya yote inaonekana kuwa sera za Donald Trump za kutaka kuzilazimisha nchi zote ziungane na Washington katika vikwazo vyake dhidi ya Iran zimegonga kisiki kutokana na upinzani mkubwa  wa kimataifa.



/129