Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Uteuzi wa Anthony Tata ulishakosoewa na maseneta wa chama cha Democrat waliomuandikia barua mapema wiki hii kumtaka ajiondoe katika uteuzi huo.
Jenerali huyo mstaafu wa jeshi, ambaye ni muungaji mkono mkubwa wa Trump, amekuwa akihudumu katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon kama mshauri mwandamizi wa waziri wake Mark Esper.
Kufutwa kikao hicho cha Seneti cha kumuidhinisha Tata kumeibua suali kama Ikulu ya White House itaamua kufuta uteuzi wake au la.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, manmo mwaka 2018 Anthony Tata aliandika jumbe kwenye mtandao wa kjamii wa Twitter akisema, Uislamu ni "dini kandamizi na ya utumiaji nguvu zaidi ninayoijua" na vile vile akamwita aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama kuwa ni "kiongozi wa kigaidi" na kumtaja kuwa ni Muislamu. Hata hivyo jumbe hizo za Twitter zilizondolewa baadaye kwenye mtandao huo.
Seneta wa chama cha Republican Jim Inhofe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Huduma Jeshini alitangaza kuahirishwa kikao cha kupitisha uteuzi wa Tata hapo jana Alkhamisi, muda mfupi kabla ya kuanza.
Hata hivyo msemaji mkuu wa Pentagon Jonathan Hoffman amesema, licha ya kukataliwa uteuzi wake, Anthony Tata ataendelea kuhudumu kama mshauri wa Esper.../
342/