27 Desemba 2021 - 11:53
Ebrahim Raisi: Wasiotupendea kheri wanafanya njama za kuvuruga uhusiano wa Iran na majirani zake

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wasiotupendekea kheri na mema, muda wote wanafanya njama za kuvuruga uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu na majirani zake.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Ebrahim Raisi amesema hayo katika kikao cha Baraza la Mawaziri la serikali yake na kuongeza kuwa, takwimu zinaonesha kwamba, usafirishaji nje bidhaa za Iran mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka jana.

Vile vile amesema, maadamu serikali ya Iran imeelekeza nguvu zake kwenye miamala ya kiuchumi na nchi jirani na kwa kweli imefanikiwa katika juhudi hizo, ni jambo lililotegemewa kabisa kuona wasiopenda jambo hilo wanazidisha njama zao za kuvuruga uhusiano wa Iran na nchi jirani, hivyo kuna wajibu wa kuwa macho sana katika jambo hilo.

Siku chache zilizopita pia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa, uhusiano wetu na Iraq ni imara na amilifu katika nyuga zote na kuna ushirikiano mkubwa baina ya nchi hizi mbili ndugu.

Hossein Amir-Abdollahian alisema hayo kupitia ujumbe wake katika mtandao ya kijamii wa Instagram na huku akigusia mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Iraq, Fuad Hussein hapa Tehran alisema, uhusiano wa Tehran na Baghdad ni wa kiistratijia kwa maana halisi ya neno.

Alisema, mabadilishano ya kibiashara na safari za mara kwa mara za viongozi wa nchi hizi mbili pamoja na wananchi wa Iran na Iraq kutembeleana muda wote bila ya kusita ni ushahidi wa wazi wa kuimarika sana uhusiano wa pande hizi mbili.

342/