27 Januari 2022 - 18:08
Ufaransa yaendeleza chuki dhidi ya Uislamu, yasema itafunga tovuti za Kiislamu

Serikali ya Ufaransa inaendeleza sera zake za chuki dhidi ya Uislamu kwa kutangaza kuwa itafunga tovuti za Waislamu kwa madai kuwa zinakiuka 'thamani za kitaifa' katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa sera ilizonazo dhidi ya uhuru wa maoni na ambazo ni kielelezo cha chuki dhidi ya Uislamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Drmanin ametangaza kuwa tovuti ya Kiislamu ya “La Voie Droite”  yamkini ikafungwa kwa kutegemea sheria za mwaka 2021 zinazohusu 'uchochezi wa chuki.

 Imetoa taarifa ya kukanusha kueneza chuki na kudai kuwa imekuwa ikiwahimiza Waislamu waheshimu wengine na kujiepusha na utumiaji mabavu.

Mwezi Julai 2021, Bunge la Ulaya lilipasisha sheria tata ambayo inawakandamiza Waislamu na kubana sheria kuhusu ufadhili wa misikiti na jumuiya za Waislamu.

Hayo yanajiri siku kadhaa baada ya Baraza la Seneti la Ufaransa kupiga kura na kuidhinisha sheria inayopiga marufuku wanawake

Waislamu kuvaa vazi la stara na heshima la Hijabu katika mashindano ya michezo. Katika miezi ya hivi karibuni Ufaransa imeshadidisha mbinyo dhidi ya Waislamu nchini humo ambapo hata maduka ya Waislamu yanafungwa kwa visingizio mbali mbali.

Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.


342/