Takwa hilo linatolewa katika hali ambayo, Sireen Mazari mmoja wa viongozi waandamizi wa chama cha Tahreek-e-Insaf ameweka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter, taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kongamano la Mayahudi wa Marekani inayokaribisha kwa mikono miwili biashara baina ya Islamabad na Tel Aviv.
Fishel bin Khalid Mpakistan mwenye asili ya Kiyahudi amedai kuwa, ametuma viungo vya chakula na matunda ya kukausha huko Palestina inayokaliiwa kwa mabavu (Israel) kupitia nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).
Pakistan ni miongoni mwa mataifa ya Kiislamu ambayo wananchi, serikali na vyama vya siasa vinapinga vikali uwepo wa utawala ghasibu wa Israel na msimamo huo umegeuka na kuwa sheria katika nchi hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni, utawala vamizi wa Israel umefanyika kila mbinu hata kupitia njia za mahusiano binafsi ili upenye nchini Pakistan.
Mansur Ahmad Khan, mweledi wa masuala ya kisiasa wa Pakistan anasema: "Wananchin wa Pakistan wanapinga vikali uwepo wa utawala dhalimu wa Israel na wangali wanasisitiza kuendelea na upinzani wao huo. Wajuzi wa mambo wa wanaamiini kuwa, upinzani dhidi ya utawala haramu wa Israel huko nchini Pakistan ni msimamo wa kitaifa. Kimsingi ni kuwa, himaya na uungaji mkono kwa malengo matukufu wananchi madhuklumu wa Palestina mkabala na Wazayuni ni miongoni mwa malengo na misimamo ya kitaifa katika nchi hiyo, na hakuna mtu anayeruhusiwa kwa namna yoyote ile kufanya mambo ambayo ni kinyume na matakwa ya wananchi wa nchi hiyo."
Licha ya kuwa, baadhi ya nchi za Kiarabu zimeamua kufuata mkondo wa usaliti kwa kuchukua ya hatua ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, lakini katika nchi hizo hizo wananchi wa nchi hizo wangali wanapinga uwepo wa utawala dhalimu wa Israel. Ni kutokana na sababu hiyon ndio maana hatua ya nchi hizo chache za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel haijawa na taathira chanya kwa utawala huo katika eneo la Asia Magharibi. Filihali utawala huo ungali unachukiwa na fikra za waliowengi katika mataifa hayo.
Huko Palestina nako pia licha ya kupitia vizazi vingi tangu ardhi za Palestina zilipokaliwa kwa mabavu, lakini upinzabni dhidi ya Wazayuni ungalipo na umekuwa ukiongezeka kila siku na kuukosesha usingizi utawala huo ghasibu. Fauka ya hayo, himaya ya kieneo na kimataifa kwa taifa madhulumu la Palestina na upinzani dhidi ya Israel ni mambo ambayo yamezidi kuuteteresha utawala huo ghasibu unaoikalia kwa mabavu Quds tukufu.
Mohsen Rouhi Sefat, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anasema: Wazayuni walikuwa ma matarajio kwamba, baada ya kupita zama za kubadilika kizazi huko Palestina basi upinzani dhidi yake utafikia tamati. Hata hivyo siyo tu kwamba, hali ya mambo haijawa kama walivyokuwa wakitarajia, bali katika mataifa mengi upinzani dhidi ya Wazayuni umeongezeka, na hii kama wanavyoamiiani wajuzi wa mambo, ni pigo kubwa kwa Israel na washirika wake.
Hivi sasa imefahamika na kueleweka wazi na bayana kwa Waislamu ya kwamba, Wazayuni kutokana na kuwa na sifa na dhati ya uvamizi, wanazitazama kwa tamaa sio ardhi za Palestina tu, bali hata ardhi za mataifa mengine hususan ya Kiislamu. Ni kwa kuzingatia ukweli huo ndio maana kama hakutachukuliwa hatua za maana na za kimsingi za kukabiliana na utawala ghasibu wa Israe, basi utawala huo utazidi kusukuma mbele gurudumu lake la uvamizi na kubakia kuwa tishio kwa mataifa mengine kutokana na siasa zake hizo za kivamizi.
342/