Shirila la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB limetangaza kuwa, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimeshambulia eneo la kusini mwa Damascus katika mji wa Aqraba (magharibi mwa Syria) kwenye barabara ya uwanja wa ndege, masafa mafupi kutoka Sayeda Zainab. Kufuatia shambulio hilo la kigaidi, Saeed Alidadi, mshauri wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran,IRGC ameuawa shahidi.Kuhusiana na hilo, jeshi la Syria limetoa taarifa na kutangaza kuwa: alfajiri ya kuamkia leo Ijumaa ndege za kivita za adui mzayuni zimefyatua makombora kadhaa kutokea kwenye anga ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na kulenga maeneo kadhaa ya kusini mwa Damascus. Hii ni sehemu ya mlolongo wa mashambulio kadhaa ya kigaidi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Syria katika wiki za hivi karibuni yakilenga kuzima wimbi jipya la mapambano ya kupigania haki ya wanamuqawama wa Palestina na Lebanon dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni. Wakati huo huo kimya cha kuaibisha cha waungaji mkono wa Kimagharibi wa utawala katili wa Israel kwa vitendo vya kigaidi vya Wazayuni hao, mbali na kudhihirisha uungaji mkono wenye maana maalumu wa Marekani na nchi za Magharibi kwa jinai hizo, kimepelekea pia kuendelezwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.../
2 Februari 2024 - 15:01
News ID: 1434550

Mshauri wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameuawa shahidi kufuatia shambulio la ndege za kivita za utawala wa Kizayuni katika mji wa Aqrabah kusini mwa mji mkuu wa Syria Damascus, karibu na eneo la Sayeda Zainab.