Mamia ya raia mjini Buenos Aires walimiminika mitaani kupinga mapendekezo ya mageuzi ya kiuchumi yaliyotangazwa na serikali ya nchi hiyo.
Magari kadhaa yamechomwa moto na waandamanaji wenye hasira pale maandamano hayo ya umma yalipogeuka kuwa ya vurugu.
Vurumai hiyo imetokea wakati wabunge wa nchi hiyo wanajadili mapendekezo ya mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyowasilishwa na Rais Javier Milei.
Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuzifuta idara kadhaa za serikali, kubinafsisha kiasi cha dazani ya mashirika ya umma ikiwemo kampuni ya ndege ya taifa na kupunguza mafao ya wastaafu sambamba na kulegeza masharti yanayotoa ulinzi kwa watu walioajiriwa.Wanasiasa wa mrengo wakushoto na vyama vya wafanyakazi nchini Argentina wanayapinga vikali mageuzi hayo wakisema kwamba, yatalirejesha nyuma taifa hilo. Hata hivyo utawala wa Rais Milei unasisitiza kwamba, mageuzi hayo ni ya lazima ili kuufufua uchumi wa Argentina unaokabiliwa na msukosuko. Sisitizo hilo la serikali limeifanya Argentina kushuhudia maandamano na vurugu hususan katika mji mkuu ambapo waandamanaji wanasisitiza kuwa, wataeandelea kuandamana mpaka takwa lao lisikilizwe.
342/