Kwa mujibu wa ripoti ya Associated Press, siku ya Jumatano kwa mujibu wa tangazo la polisi wa Las Vegas Kaskazini iliyoko katika jimbo la Nevada, mshukiwa wa mauaji ya watu watano alijiua baada ya kukabiliana na polisi wa eneo hilo.
Katika taarifa hiyo, polisi wa Las Vegas walimtaja mshukiwa huyo kuwa ni Eric Adams mwenye umri wa miaka 47 kwamba, ndiye aliyefanya mashambulizi hayo ya kutisha huko Las Vegas, Marekani. Kulingana ripoti walizotoa polisi, tukio hilo lilitokea siku ya Jumatatu usiku na mshukiwa alijaribu kukimbia baada ya kutambuliwa na kisha kujiua. Adams alikuwa akishukiwa kuwapiga risasi na kuwaua wanawake wanne na mwanamume mmoja katika majengo mawili tofauti katika eneo la makazi la North Las Vegas huko Marekani. Na vile vile, kwa mujibu wa uthibitisho wa polisi, msichana wa miaka 13 pia alijeruhiwa kwa risasi na yuko katika hali mbaya.
Matokeo mapya ya uchunguzi mpya uliofanywa na Taasisi ya Kaiser Family nchini Marekani yanaonyesha kuwa, mtu mmoja kati ya kila watu watano nchini Marekani ametishwa kwa silaha na kukabiliwa na utumiaji mabavu wa silaha. Kila mwaka, maelfu ya watu huuawa au kujeruhiwa kutokana na ufyatuaji risasi katika miji tofauti ya Marekani. Kwa kulingana na ripoti rasmi, kuna takriban bunduki milioni 270 hadi 300 nchini Marekani; Ina maana kwamba kuna karibu bunduki moja kwa kila mtu katika nchi hiyo.
342