Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuhusu jaribio la kumuua Donald Trump wakati wa hotuba yake katika mkutano wake wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Pennsylvania, Marekani.
Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari vya Marekani, mtu mmoja alimpiga risasi Trump, lakini risasi hiyo iligonga sikio lake la kulia na kumfanya atokwe na damu upande wa sikio.
