Jeshi la Kizayuni limetangaza katika taarifa yake kuwa wanajeshi wake wawili wameuawa na wengine wanne wakiwemo maafisa wawili wamejeruhiwa vibaya katika mapigano na wanamapambano wa Kipalestina katika Ukanda wa Ghaza.
Jeshi la utawala wa Kizayuni limetoa taarifa hiyo baada ya Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Hamas kutangaza jana Alkhamisi kuwa wapiganaji wake wamevilenga vitengo viwili vya jeshi la Israel kusini mwa Ghaza, na kuwaua na kuwajeruhi wanajeshi kadhaa.
Taarifa ya Al-Qassam imesema, wapiganaji wake waliwashambulia wanajeshi saba wa Israel kwa mada zenye miripuko mikubwa karibu na Msikiti wa Omar ibn Abd al-Aziz katika kitongoji cha al-Tannour mashariki mwa Rafah.Brigedi za Al-Qassam ziliripoti hapo awali kwamba zililenga kitengo cha uhandisi cha Israel cha wanajeshi 12 kilichokuwa kikijiandaa kutekeleza operesheni ya ubomoaji ndani ya nyumba karibu na makutano ya al-Fidai katika kitongoji hicho.
Taarifa ya Al-Qassam imesema, mripuko uliotokea ndani ya nyumba hiyo ulisababisha vifo vingi, na kwamba brigedi hizo ziliona helikopta za Israel zikitua eneo la tukio kuwaondoa maiti na majeruhi.../
342/
Your Comment