al-Houthi amelaani ghasia zinazoendelea Gaza, na kuzitaja kuwa "uhalifu wa karne." Kiongozi huyo wa Ansarullah ya Yemen ameonyesha masikitiko makubwa kutokana na mwitikio hasi wa mamilioni ya Waislamu kwa ukatili wa kila siku unaowakabili watu wa Palestina. Matamshi ya Al-Houthi ni kilio cha hadharnia kwa Ummah wa Kiislamu kuamka katika majukumu yao na kuchukua msimamo dhidi ya dhulma.
Al-Houthi amesisitiza kuwa, adui anaendeleza mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Gaza kwa muda wa mwezi wa kumi na tisa mfululizo hukuu dunia ikishindwa kuchukuua hatua za maana kusitisha jinai za Israel.
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesikitishwa na uzembe wa Waarabu na Waislamu katika majukumu yao matukufu yakiwemo ya jihadi na kusimama dhidi ya dhulma.
Ameonya kwamba kupuuza matukio haya hakutauepusha Umma na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na kwamba, ukimya huu utakuwa na matokeo mabaya mbele ya Mwenyezi Mungu. Aidha ameashiria kuwa, utawala wa Kizayuni unayalenga mataifa yote na kutaka kuyaangamiza kabisa huku akiwataka Waislamu kutambua tishio la pamoja na kuungana dhidi yake.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, asasi mbalimbali za kimataifa zimeendelea kuonya kuhusiana na hali mbaya ya uhaba na ukosefu wa chakula katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, hivi sasa maghala ya chakula katika ukanda huo yapo tupu.
342/
Your Comment