FBI imeongeza kuwa, haikuwa na taarifa za awali kuhusu kuwepo tishio kwa mkutano wa kampeni wa Trump, ambako alikuwa akitoa hotuba.
Idara ya Upelelezi ya Marekani imesisitiza kwamba, inaendelea kufanya uchunguzi na upekuzi wa maeneo yanayotiliwa shaka, magari na maeneo yanayohusiana na tukio hili.
FBI imemtambulisha mpiga risasi huyo kuwa ni Thomas Matthew Crooks mwenye umri wa miaka 20, kutoka Bethel Park huko Pennsylvania.
FBI imeongeza kuwa, uchunguzi unaendelea kubaini sababu za jaribio la mauaji lililosababisha kuuawa mhalifu na mmoja wa watu waliokuwa eneo hilo, na vilevile kujeruhi vibaya wengine wawili.
Kwa upande wake, shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa Crooks alisajiliwa na chama cha Republican, kulingana na rekodi za wapiga kura.
Kwa upande wake, polisi ya Pennsylvania imesema kwamba uchunguzi wa tukio la kupigwa risasi Donald Trump unaweza kuchukua miezi kadhaa.
Imeongeza kuwa kipaumbele ni kujua sababu zilizopelekea kupigwa risasi rais huyo wa zamani wa Marekani, na kama kuna watu wengine waliohusika katika hujuma hiyo.
Video ya moja kwa moja kutoka eneo la tukio ilimuonyesha Trump akivuja damu upande wa kulia wa uso na sikio lake. Trump alionekana akiweka mkono wake sikioni kabla ya kuanguka chini nyuma ya jukwaa.
342/