16 Julai 2024 - 21:28
Jaribio la mauaji Pennsylvania: Ni mchezo wa kuigiza au mbinu ya propaganda ya Trump?

Tukio la kujeruhiwa sikio rais wa zamani wa Marekani na mgombea wa sasa wa chama cha Republican, Donald Trump, alipokuwa akihutuba mkutano wa kampeni za uchaguzi huko Pennsylvania siku ya Jumamosi ya juzi limeibua maswali mengi baina ya wanasiasa na wanadau wa mitandao ya kijamii.

Picha za video zilionyesha kuwepo milio mingi ya risasi wakati wa hotuba ya Trump, na pia damu ikichuruzika kwenye sikio lake la upande wa kulia.

Baada ya kusambaa viodeo hizo, wachambuzi wa siasa na watumiaji wa mitandao ya kijamii walianza kuchambua yaliyojiri na kueleza mitazamo tofauti kuhusu kilichotokea, na iwapo ni mchezo wa kuigiza au jaribio la kweli la mauaji?

Baadhi ya wachambuzi wameeleza kilichotokea kuwa ni mchezo wa kuigiza ulioratibiwa na kambi ya Trump ili kuboresha nafasi yake ya kushinda katika uchaguzi ujao wa rais wa Marekani mwezi Novemba mwaka huu.

Wametia nguvu hoja yao kwa mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kwamba baada ya msururu wa risasi, moja tu ndiyo "iliyomkuna" sikio Trump, na baada ya hapo aliondoka kwenye mkutano huo wa kampeni huku akiinua mkono juu na kushangiliwa na wafuasi wake.
Mmoja kati ya watumiaji wa mitandao ya kijamii amesema, yumkini risasi iliyotumiwa kujeruhi sikio la Trump ilikuwa ya plastiki na kwamba, lau angepigwa risasi halisi, ingerarua sikio lake, na sauti yenyewe ya risasi ingeathiri usikivu wake kwa muda mrefu, si sekunde chache tu. Kwa upande mwingine, baadhi ya waangalizi wa mambo wamepinga mtazamo huo wakisema kwamba kilichotokea kwa Donald Trump ni jaribio halisi la mauaji, na ushahidi ni risasi ya kwanza iliyopita karibu na sikio lake, na ya pili ilipiga fulana yake ya kujikinga na risasi. Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) imethibitisha leo Jumapili kwamba shambulizi dhidi ya rais wa zamani na mgombea wa sasa, Donald Trump, huko Pennsylvania jana jioni lilikuwa jaribio la mauaji, na kwamba imemtambua mpiga risasi aliyeuawa, huku uchunguzi ukiendelea.


342/