Donald Trump, alipigwa risasi na kujeruhiwa kidogo siku ya Jumamosi, Julai 13, alipokuwa akizungumza katika kampeni ya uchaguzi huko Butler, katika jimbo la Pennsylvania.
Mshambuliaji aliyejaribu kumuua Trump aliuawa papo hapo na polisi wa Marekani katika eneo la tukio, na hivyo kuondoa uwezekano wa kuhojiwa ili kubaini wahusika wa tukio hilo.
Amir Saeid Iravani, Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa mjini New York alisema jana Jumanne, akijibu ripoti zinazodai kuwa Iran ilihusika katika jarihio hilo la mauaji, kwamba tukio la kupigwa risasi Trump linaweza kutathminiwa kama ishara nyingine ya kuongezeka kila siku ghasia za kisiasa nchini Marekani katika miaka ya hivi karibuni, hasa baada ya kushambuliwa Bunge la Congress ya Marekani na wafuasi wa Donald Trump Januari tarehe 6, 2021.
Jibu la Iran kuhusu ripoti zinazodai kuwa Iran ilihusika katika jaribio la kumuua Donald Trump, linaeleza kuwa uchunguzi wa historia ya Marekani unaonyesha wazi kuwa viongozi wa kisiasa na wanaharakati wa kisiasa na kijamii wa nchi hiyo daima wamekuwa wakilengwa na ghasia za kisiasa na mauaji ya kigaidi. Mfano wa wazi wa suala hili ni mauaji ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya Rais John F. Kennedy wa Marekani, huko Dallas, Texas, Novemba 1963, mauaji ya Robert Kennedy, mgombea wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa rais wa Marekani, Juni 1968 mjini Los Angeles, California na mauaji ya Martin Luther King, kiongozi wa harakati ya haki za kiraia mwenye asili ya Kiafrika huko Memphis, Tennessee mnamo Aprili 1968. Amir Saeid Iravani, Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Donald Trump, ni mtendajinai anayepaswa kuhukumiwa na kuadhibiwa mahakamani kwa kutoa amri ya kuuawa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), aliyeuawa shahidi Januari 3, 2020. Kuhusiana na suala hilo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechagua njia ya kisheria ya kumuwajibisha Trump.
342/