Lavrov aliyasema hayo jana Jumatano katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matukio ya Asia Magharibi, ikiwa ni pamoja na kadhia ya Palestina na kusema kuwa Ukanda wa Gaza unashuhudia kusambaratika kwa miundombinu yake kutokana na mashambulio ya kikatili yanayofanywa kila siku na utawala ghasibu wa Israel katika ukanda huo.
Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Russia amesema Russia inapinga kile kinachoendelea huko Gaza ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya watu wasio na hatia. Amesisitiza kwamba Wapalestina wanapaswa kupewa fursa ya kujiamulia hatima yao wenyewe bila ya kuingiliwa na nchi za kigeni. Licha ya upinzani wa kieneo na kimataifa, utawala bandia wa Israel unaoua watoto wa Kipalestina umekuwa ukishambulia Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7, Oktoba mwaka jana ambapo Marekani ni miongoni mwa watoaji wakubwa wa silaha kwa utawala huo ghasibu. Marekani inaupa silaha utawala wa Kizayuni katika hali ambayo utawala huo ghasibu umeshindwa kufikia malengo yoyote katika vita vyake huko Gaza na pia umepoteza uungaji mkono wa kimataifa kutokana na kuendeleza jinai za kinyama dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
342/