Qura’ni inasema:
«.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا … لَا يَغْتَبْ بَعْضُكُمْ بَعْضًا أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَنْ يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَحِيمٌ»
“Enyi mlio amini! … msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.” (Hujurat 49:12)
Kwa nini Ghibah (kusengenya) imefananishwa na kula nyama ya ndugu yetu aliyekufa?- Kwanza, mtu aliyekufa hawezi kujitetea. Kadhalika, mtu anayesengenywa hayupo ili aweze kujitetea.
- Kusengenya kunaharibu heshima ya mtu na hiyo hailipiki. Kama nyama ya mtu aliyekufa, iliyoraruliwa, haiwezi kuponywa.
- Nyama hukua kwa muda na taratibu. Kadhalika, sifa ya mtu huchukua muda mrefu kuendelezwa.