Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Venezuela imetangaza katika taarifa yake kwamba, Caracas imeamua kuwaita nyumbani wanadiplomasia wake kutoka katika nchi za Chile, Argentina, Costa Rica, Peru, Panama, Jamhuri ya Dominika na Uruguay kutokana na ada isiyo sahihi ya nchi hizo ya kutotambua ushindi wa Nicolas Maduro katika uchaguzi wa rais.
Wakati huo huo, wapinzani wa Maduro wenye mielekeo ya Kimagharibi pia wanajaribu kutumia vurugu na machafukko ili kupinga ushindi wa Maduro katika uchaguzi huo ambapo wanadai kumefanyika wizi na udanganyifu. Ni kutokana na sababu hiyo, ndio maana serikali ya Caracas imelaani na kusisitiza kwamba, misimamo ya nchi hizo kuhusu uchaguzi wa rais wa Venezuela ni uingiliaji wa masuala ya ndani ya nchi hiyo. Taarifa ya serikali ya Venezuela imesisitiza kuwa, taifa hilo lina haki ya kuchukua hatua za kisiasa na kisheria ili kulinda wa haki na mamlaka yake ya kujitawala.
Aidha taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Venezuela itapinga harakati zozote zinazotishia kuishi pamoja kwa amani. Marekani inaonekana kuwa na hasira zaidi kuliko nchi nyingine yoyote ile kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais wa Venezuela. Ni kutokana na ukweli huo, ndio maana, wapinzani wa Maduro wenye mielekeo ya Kimagharibi walianzisha vurugu na fujo mara tu baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo.
342/