21 Oktoba 2024 - 11:37
Uchoraji wa ukutani wa Sura ya Syed Hassan Nasrullah katika Mji Mkuu wa Venezuela

Katika hafla ya uzinduzi wa mchoro wa (sura) uso wa Syed Hassan Nasrullah, mche wa mti pia ulipandwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Syed Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon aliyeuawa Kishahidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Kwa lengo la kuenzi umri wa maisha ya mapambano ya Syed Hassan Nasrullah dhidi ya adui Mzayuni, (sura au) uso wa Katibu Mkuu wa Hezbollah aliyeuawa Kishahidi wa Lebanon, ulichorwa kwenye moja ya kuta za Mji Mkuu wa Venezuela.

Akizungumzia kujitolea kwake (kumchora kwa irada yake) mtu huyu mkubwa (Syed Nasrullah), mchoraji wa kazi hii ya kisanaa alisema kuwa anamchukulia Syed Hassan Nasrullah kuwa ni kielelezo chenye thamani kwa watu wote wapenda uhuru, na akataja madhumuni ya kuunda (na kubuni) kazi hii ya kisanaa kuwa ni ili kutoa fursa kwa wapita njia kumkumbuka Syed Hassan Nasrullah katika Mji huu wa Caracas kupitia kuona uso huu (na sura hii ya Syed Hassan Nasrullah).

Tangu kuanza kwa jinai za Utawala Haram wa Kizayuni, daima Serikali na Wananchi wa Venezuela wamekuwa wakiwaunga mkono Wananchi madhulumu wa ‘Palestina na Lebanon’ kwa kulaani jinai hizo na kutaka kuadhibiwa kwa ‘Netanyahu’ na wale wote waliohusika na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia (katika nchi hizo).

Katika hafla ya kuzindua mchoro wa (sura) uso wa Syed Hassan Nasrullah, mche wa mti ulipandwa pia kwa ajili ya kumbukumbu ya Katibu Mkuu wa Hezbollah aliyeuawa Kishahidi.