31 Desemba 2024 - 04:21
Ujerumani yazindua kituo cha kwanza cha kupambana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu

Moja ya majimbo ya Ujerumani yenye watu wengi zaidi itazindua kituo cha kwanza cha kumbukumbu za matukio kuhusu ubaguzi wa rangi dhidi ya Uislamu katika msimu ujao wa kuchipua.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Jimbo la North Rhine-Westphalia ndilo jimbo lenye watu wengi zaidi nchini Ujerumani, ambalo lina zaidi ya wakazi milioni 1.7 wa Kiislamu, na kituo hiki, kinachoitwa " MEDAR", azimio lililopo ni kufunguliwa kwake.

Madhumuni ya kufungua kituo hiki ni kuandika na kuripoti mashambulizi na jinai dhidi ya Waislamu.

Kituo hicho, ambacho kinaendeshwa na Serikali ya jimbo hilo, pia kinafuatilia vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya wageni wasio Waislamu, kituo cha habari cha WDR kiliripoti.

Kituo hiki, kitakachofunguliwa Mwezi Machi au Aprili 2025, ni matokeo ya miaka 3 ya ufuatiliaji na maandalizi yake.

Jimbo la Rhine Kaskazini-Westphalia, jimbo lenye watu wengi zaidi nchini Ujerumani lenye watu zaidi ya milioni 18, litakuwa jimbo la kwanza nchini humo kufungua kituo cha aina hiyo ili kuripoti matukio ya chuki (na ubaguzi) dhidi ya Waislamu.

Jimbo hilo limeshuhudia mashambulizi kadhaa dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya ibada.

Mnamo Januari 2022, makaburi kadhaa ya Waislamu yaliharibiwa katika jiji la Izloun Mnamo April 2022, Serikali pia ilianzisha Kituo cha Kupambana na Uyahudi kwa lengo la kuweka kumbukumbu za matukio yanayohusiana (na hilo) katika eneo lote.