12 Agosti 2025 - 22:40
"Sifa Sita za Muumini Zinazomhakikishia Pepo"

Maelezo yafuatayo yanaeleza matendo au sifa sita ambazo kuyatekeleza kunaweza kusababisha wokovu na kuingia peponi. Mambo haya sita ni nguzo za msingi za maisha ya kiimani na yenye kujitolea. Maandiko haya yanalenga, kwa kuyataja mambo haya, kutoa njia iliyo wazi kuelekea kwenye furaha ya Akhera.

Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema:
«Tukubalieni mimi mambo sita, nami nitawakubalia pepo; mnapozungumza, msiseme uongo; na mkiahidi, msivunje ahadi; na mkiaaminiwa, msisaliti; shusheni macho yenu; jihifadhini na maasi ya zinaa; na zuieni mikono yenu na ndimi zenu.»[1]

Maneno ya Maimamu watoharifu (a.s) ni mwongozo wa maisha yetu na yanaonyesha mtindo wa maisha ya kidini. Hadithi hii iliyopokewa kutoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w) ni mkusanyiko wa mema yote kwa mwanadamu. Mtume (s.a.w) katika hadithi hii amesema kuwa kuna sifa sita ambazo mkizikubali, mimi nitawakubalia pepo. Maana ya maneno ya Mtume (s.a.w) ni kuwa mkizingatia masharti haya sita na kuyatekeleza, matokeo yake ni kupata pepo.

Bila shaka vipo vishawishi vya Shetani na matamanio ya nafsi, lakini ikiwa mtu atakuwa na azma thabiti na kufanya maamuzi kulingana na azma hiyo, utekelezaji wa masharti haya utakuwa rahisi na unaowezekana. Walii wa Mwenyezi Mungu [mbali na Mitume na Maimamu watoharifu (a.s)] walikuwa watu kama sisi, lakini kwa uimara wa azma waliouonyesha, waliukanyaga Shetani na matamanio ya nafsi na wakafikia daraja la ukaribu na Mwenyezi Mungu.

Mtume (s.a.w) katika hadithi hii amesema: Kubalianeni nami mambo sita [na mtekeleze], nami nitawakubalia pepo [yaani nitawahakikishia pepo]:

1- La kwanza: Mnapozungumza, msiseme uongo.
Kusema uongo kunapoteza imani ya watu kwako; mfano, mtu akimdanganya mke na watoto wake, wataacha kumuamini, na kurejesha uaminifu uliopotea ni jambo gumu. Uongo ni tatizo ambalo limeenea katika jamii na kwa baadhi limekuwa mazoea, kiasi kwamba hawawezi kuacha kusema uongo. Hii inasababisha mtu apoteze heshima machoni pa watu wengine na kujulikana kama mtu wa hadaa.

2- La pili: Mkiahidi, msivunje ahadi.
Kuvunja ahadi pia kunapoteza imani ya watu. Ikiwa mtu ameahidi, kwa mfano, kurudisha fedha alizokopa katika muda fulani, basi azirudishe katika muda huo, si kuahirisha kwa visingizio mbalimbali. Hata kwa mke na watoto, mtu asitoe ahadi asiyo na uwezo wa kuitekeleza, kwa kuwa watoto hujifunza kutoka kwa wazazi wao, na wakiona wazazi wanavunja ahadi, nao wataiga tabia hiyo. Ikiwa mtu atashindwa kutimiza ahadi, basi aombe radhi mara moja kwa kuchelewesha.

3- La tatu: Mkikabidhiwa amana, msisaliti.
Mtu lazima awe mwaminifu kwa amana aliyopewa, iwe ni ya mali au ya kijamii (wajibu wa kijamii).

4- La nne: Fungeni macho yenu na muepuke kuangalia mambo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu.
Muumini ana haya na sitara, na haangalii kila kitu.

5- La tano: Jihifadhini na uchafu wa zinaa.

6- La sita: Zuieni mikono yenu na ndimi zenu.
Kudhibiti mikono na ndimi ni jambo muhimu sana. Mojawapo ya matatizo makubwa ya jamii ni kutotunza ulimi, kiasi kwamba wengine hawasiti hata kuharibu heshima za wengine.

Vyanzo:

1. Allama Majlisi (Muhammad Baqir), Bihar al-Anwar (toleo la Beirut), juz. 68, uk. 286; Muhammad bin Ali, Ibn Babawayh (Sheikh Saduq), al-Amali, uk. 90.

Tovuti ya Shia Quest.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha