Majid Takht Ravanchi amesema: "Vitisho kutoka kwa Marekani na utawala wa Kizayuni si jambo jipya, lakini wanajua nguvu halisi ya Iran."
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kushikamana serikali ya Iran na mfumo jumla uliowekwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Marekani.
Takht Ravanchi ameongeza kuwa: "Wakati wa uongozi wa Rais Rouhani, baada ya mazungumzo magumu na tata, tulifikia mapatano ambayo serikali ya Marekani haikuyaheshimu, si katika kipindi cha rais wa zamani Barack Obama wala muhula wa kwanza wa utawala Donald Trump, na hatupaswi kusahau historia hii."
Takht Ravanchi, hata hivyo, amesema mazungumzo yanaendelea kati ya Iran na nchi tatu za Ulaya zilizotia saini mkataba wa nyuklia wa JCPOA mwaka 2015.
342/
