Mohammed Bagher Ghalibaf amesema hayo katika mazungumzo yake na Tariq Hameed Naibu Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pambizoni mwa Kikao cha 15 cha Bunge la Asia (APA) na kusisitiza juu ya udharura wa kuungana na kuwa kitu kimoja mataifa ya Kiislamu dhidi ya vitisho vya maadui.
Ghalibaf ameashiria jinai zinazofanywa na Wazayuni kwa uungaji mkono wa Marekani na kutoa wito wa kuimarishwa uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kibunge kati ya Iran na Imarati. Kadhalika Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea kufurahishwa kwake na kuundwa serikali mpya nchini Lebanon na akabainisha kwamba, ana matumaini kuwa serikali halali pia itaundwa huko Gaza.
Qalibaf ameashiria kuuawa watu zaidi ya 50,000 katika jinai zilizofanywa na utawala haramu wa israel huko Gaza Palestina na Lebaon na kubainisha kwamba, ni fedheha kubwa.
Amesema kuna haja ya kuweko ushirikiano wa karibuu baina ya mataifa ya Kiislamu kwa ajili ya kudhamini amani na usalama wa kudumu.
Kwa upande wake Hameed Tariq Naibu Spika wa Bunge la Imarati amesisitiza urafiki na udugu baina ya Iran na Imarati na kutoa mwito wa kukuzwa ushirikiano wa kiuchumi na kiutalii.
342/
