20 Februari 2025 - 19:58
Hamas: Israel iliua mateka wake kwa kulipua vituo walikokuwa wamezuiliwa

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema leo Alkhamisi kwamba, tawi lake la kiijeshi Izuddin al Qassam na muqawama kwa ujumla vina wamefanya kila liwezekanalo kulinda heshima ya maiti wakati wa shughuli ya kukabidhi miili ya matekka hao, ilhali utawala vamizi wa Isarel haukuheshimu uhai yao walipokuwa hai.

Taarifa iliyotolewa na Hamas kabla ya kukabidhi miili ya wateka 4 wa Israel kwa mujibu wa masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, imesema kwamba Hamas ililinda uhai na maisha ya mateka wa Waisraeli katika Ukanda wa Gaza, ikawapa kile ilichoweza na kuwatendea ubinadamu, lakini jeshi lao la Israel liliwaua pamoja na watekaji wao.

Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa jeshi la Israel liliwaua mateka wake kwa kulipua vituo walikkokuwa wamehifadhiwa, na serikali ya Tel Aviv inapaswa kuwajibika baada ya kukwamisha mara kwa mara makubaliano ya kubadilishana mateka.

Hamas isema kwamba mhalifu Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anajiliza mbele ya miili ya mateka wake katika jaribio la wazi la kukwepa kuwajibika kwa mauaji yao mbele ya umma.

Msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas, Abu Obaida amesema: Mateka wote walikuwa hai, "kabla ya maeneo walikokuwa wakishikiliwa kulipuliwa kwa makusudi na ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel."

Hamas pia imetuma ujumbe kwa familia za watoto wawili, Bibas na Lifshitz ikisema: "Tulipendelea kuona watoto wenu wakirudi wakiwa hai, lakini viongozi wenu walichagua kuwaua pamoja na watoto 17,881 wa Kipalestina."

Leo, Shirika la Msalaba Mwekundu limepokea miili ya mateka wanne wa Israel katika Makaburi ya Mashahidi katika eneo la Bani Suhaila huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

342/