21 Februari 2025 - 18:03
IAEA: Tumekubaliana na Iran tuendeleze falsafa ya mapatano ya JCPOA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema katika mazungumzo na waandishi wa habari mjini Tokyo Japan kuwa: "Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwamba "falsafa ya JCPOA" ambayo msingi wake ni "kuchukua Iran hatua za hiari mkabala wa kupewa upendeleo na motisha," inaweza kuendelea.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Russia, TASS, Rafael Grossi, amesema hayo mbele ya wandishi wa habari mjini Tokyo Japan na kujibu swali kuhusu mapatano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina la "Mpango Kamili wa Utekelezaji (JCPOA) na kusisitiza kuwa, vipengee vya mkataba huo hivi sasa vimeshakuwa vya zamani hivyo ni lazima tutafute muundo mpya wa makubaliano ya nyuklia na Iran.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa IAEA amesema: "JCPOA ni ganda tupu. Nadhani hakuna mtu anayefikiria hivi sasa kwamba JCPOA inaweza kufanya jambo lenye taathira. Nadhani haya ni makubaliano ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu. Na kwa sasa bila ya kujali kwamba yana faida au hayana, ni wakati wake wa kutafutwa mbadala." Kwa mujibu wa Grossi, maandishi yaliyomo kwenye makubaliano ya JCPOA yana habari zilizopitwa na wakati, zikiwemo aina za vinu vya nyuklia vinavyotumiwa na Iran. Mkurugenzi Mkuu wa IAEA amesemapia kwamba: Katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi, pande hizo mbili zimekubaliana kwamba "falsafa ya JCPOA" ambayo msingi wake ni Iran kuchukuua hatua za hiari mkabala wa kupewa upendeleo na motisha, inaweza kuendelea.

Vile vile amerejea madai yao ya kila siku ambayo yamekuwa yakikanushwa mara kwa mara na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambao muda wote wanasisitiza kwamba Tehran haina nia kabisa ya kumiliki silaha za nyuklia na kusema, "Iran lazima ithibitishe haitaki silaha za nyuklia."

342/