Jenerali Nasirzadeh amesema kuwa tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maadui wamekuwa wakipanga njama dhidi ya Iran. Ameongeza kuwa walilazimisha Iran kuingia vitani, lakini vita hivyo vilipelekea ukuaji na kujitegemea kwa nchi, na sasa Iran imekuwa muuzaji wa silaha, ilhali wakati mmoja hata waya yenye miiba haikuruhusiwa kuingizwa ndani ya nchi.
Jenerali Nasirzadeh amefafanua sababu za uadui wa Marekani na mataifa mengine makubwa dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kwa kusema mapinduzi haya yamekuwa yakipinga madhalimu na watawala wa kidikteta tangu mwanzo. Ameendelea kusema kuwa mapinduzi haya yalianza na kukua chini ya uongozi wa Imam Khomeini (RA) na yamekuwa katika mgongano wa kiasili na madola makubwa kama Marekani, kwa sababu Iran inapinga udhalimu na ukandamizaji.
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa leo, fikra za kimapinduzi za Iran zimekuwa na athari katika ngazi ya kimataifa, na maadui wanahofia jambo hili.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Jenerali Nasirzadeh alimsifu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa jukumu lake la busara na la hali ya juu katika kusukuma mbele malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu.
342/
