Rais Masoud Pezeshkian ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: Taifa kubwa la Lebanon linastahili kujivunia watoto wake wote majasiri hasa viongozi hawa wawili mashujaa ambao waliheshimu viapo vyao na kutetea heshima ya taifa la Lebanon hadi wakauawa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu.
"Tutaendelea kutii viapo tulivyokula."
Wakati huo huo mamia ya maelfu ya waombololezaji kutoka maeneo mbalimbali ya ukanda wa Asia Magharibi na maeneo mengine duniani wamemiminika katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut kwa ajili ya kushiriki katika mazishi ya Sayyid Hassan Nasrullah, kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu wa harakati ya Hizbullah, na mrithi wake aliyeteuliwa baada yake, Sayyid Hashim Safiyudddin, ambao wote waliuliwa shahidi na utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka jana.
Waombolezaji wameminika katika uwanja wa michezo wa Camille Chamoum na katika mitaa jirani ya kusini mwa Beirut. Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah atazikwa leo Jumapili huko Burj al Barajneh katika kitongo cha kusini mwa Beirut, na Sayyid Safiyuddin atazikwa kesho Jumatatu katika eneo anapotoka la Deir Qanoun.
342/
