23 Februari 2025 - 19:26
Familia ya Bibas yakataa kuwaruhusu mawaziri wa serikali ya Netanyahu kuhudhuria mazishi yake

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa familia ya Shiri Bibas imesema kiongozi yeyote wa serikali ya Benjamin Netanyahu hapaswi kuhudhuria mazishi ya wana wao watatu, ambao miili yao ilirejeshwa siku chache zilizopita huko Israel kutoka Ukanda wa Gaza.

Tovuti ya Israel, Walla imeripoti kwamba mawaziri wa serikali ya Israel waliarifiwa kwamba familia ya Bibas haitaki mwakilishi wa serikali kushiriki katika mazishi ya wanafamilia hao.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) lilikabidhi kwa jeshi la Israel miili ya Bibas na watoto wake wawili, Ariel na Kfir pamoja na mwili wa mateka mwingine, Oded Lifshitz.

Siku ya Ijumaa, familia ya Bibas ilimtuhumu Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuwa "amewatelekeza" ndugu zao watatu baada ya shambulio la Oktoba 7, 2023, na kwamba ameshindwa kuwarudisha salama.

Katika taarifa yake, Hamas imeeleza kwamba, mateka hao wa Israel waliuawa katika mashambulizi ya kiholela ya anga yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni wakati wa vita vya mauaji ya kimbari vya miezi 15 dhidi ya eneo lililowekewa mzingiro la Ukaknda wa Gaza.

Msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas, Abu Obaida amesema: Mateka wote walikuwa hai, "kabla ya maeneo walikokuwa wakishikiliwa kulipuliwa kwa makusudi na ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel."

Hamas pia imetuma ujumbe kwa familia za watoto wawili, Bibas na Lifshitz ikisema: "Tulipendelea kuona watoto wenu wakirudi wakiwa hai, lakini viongozi wenu walichagua kuwaua pamoja na watoto 17,881 wa Kipalestina."

342/