23 Februari 2025 - 19:27
Waziri Mkuu wa Yemen: Hizbullah imempigisha magoti adui Mzayuni

Waziri Mkuu wa Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi ya Yemen amesema kuwa Harakati ya Muqawama ya Lebanon, Hizbullah, imempigisha magoti adui Mzayuni.

Ahmad al Rahawi ameeleza kuwa, harakati ya Hizbullah imeimarika zaidi mara zote ilipowatoa mhanga makamanda wake.

Al Rahawi ameongeza kuwa: Hizbullah hii leo imekuwa nguvu ya kikanda inayowahami na kuwatetea watu wanaodhulumiwa hususan wananchi wa Palestina.

Amesema: Watu wote leo, wakati wa mazishi makubwa ya mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Saffiyuddine katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, watashuhudia jnguvu na ukubwa wa harakati ya Hizbullah.

Ameongeza kuwa Shahidi wa Umma wa Kiislamu, shahidi wa Uislamu na ubinadamu Sayyid Hassan Nasrallah na Shahidi Sayyid Hashem Safiyuddin ni nembo ya uhuru, kujitawala, kutetea haki na mapambano dhidi ya batili.

Waziri Mkuu wa Yemen amesema: Sayyid Hassan Nasrullah alikuwa shakhsia wa kwanza aliyeitetea Yemen wakati ilipokabiliwa na mashambulizi na uvamizi wa Saudi  Arabia na Marekani. 

Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa zamani wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon na aliyekuwa makamu wake, Sayyid Hashim Safiyuddin watazikwa lao Jumapili na kesho Jumatatu kwa utaratibu.

Nasrullah atazikwa huko Burj al Barajneh katika kitongoji cha kusini mwa Beirut, na Sayyid Safiyuddin atazikwa  katika eneo anapotoka la Deir Qanoun. 

Sayyid Hassan Nasrullah aliuawa shahidi katika jinai iliyotekelezwa na utawala ghasibu wa Israel katika eneo la Dhahiyeh kusini mwa Beirut siku ya Ijumaa tarehe 27 Septemba mwaka jana. 

342/