23 Februari 2025 - 19:28
Iran kuwakilishwa na Spika wa Bunge, Waziri wa Mambo ya Nje katika mazishi ya Shahidi Nasrallah

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) Mohammad Baqer Qalibaf na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi leo wanaelekea Beirut kushiriki katika hafla ya mazishi ya kiongozi wa Hizbullah aliyeuawa shahidi, Sayyed Hassan Nasrallah, pamoja na mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, Shahidi Sayyid Hashim Safieddine.

Araghchi na Qalibaf, wakiwa wameandamana na wabunge kadhaa watawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rafic Hariri jijini Beirut Jumapili asubuhi kushiriki katika msafara wa mazishi, ambayo yamepangwa kufanyika kuanzia saa saba mchana kwa saa za Beirut.

Sayyid Nasrallah aliuawa shahidi katika mashambulizi ya kigaidi ya anga yaliyotekelezwa na utawala haramu wa Israeli kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27, 2024.

Kwa kutumia tani 85 za vilipuzi, ndege za kivita za Israeli ziliharibu majengo sita ya makazi huko Dahiyeh, kufuatia kampeni ya wiki moja ya mashambulizi dhidi ya maeneo mengi kutoka kusini mwa Lebanon hadi Beirut.

Naye Sayyid Safieddine aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la Israel mnamo Oktoba 2024.

Harakati ya Hizbullah iliahirisha hafla ya mazishi ya viongozi hao wawili kutokana na hofu ya mashambulizi ya Israel wakati wa kuwaaga mashahidi hao katika kipindi cha vita.

Sasa, zaidi ya miezi mitano baada ya mashambulizi hayo ya kigaidi, uwanja wa ndege wa Beirut na mitaa yake inashuhudia misafara mkubwa ya watu, wengi wakipeperusha bendera za Hizbullah na kubeba picha za mashahidi hao wawili.

Jumanne, afisa wa Hizbullah alisema kwamba wajumbe kutoka nchi 79 watahudhuria hafla ya mazishi ya mashahidi Nasrallah na Safieddine inayofanyika leo.

342/