Taarifa iliyotolewa na Vatican imesema: "Papa Francis, ambaye amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki moja kutokana na matatizo ya kupumua ambayo yamesababisha nimonia katika mapafu yote mawili, bado yuko katika hali "mbaya" na amepata "tatizo la pumu ya kupumua."
Vyanzo vya habari vya Vatican vinasema kuwa Papa anahitaji oksijeni ya ziada ili kupumua, vikieleza kuwa hata hivyo, moyo wake umesalia katika hali nzuri hadi sasa.
Hii ni mara ya nne kwa Papa kulazwa hospitalini tangu 2021, na hali yake inatia wasiwasi baada ya kukumbwa na orodha ndefu ya matatizo ya kiafya katika miaka ya nyuma, ikiwa ni pamoja na upasuaji wa utumbo na matatizo ya kutembea.
Hali ya kiafya ya sasa ya Papa Francis inaripotiwa kuwa ndiyo mbaya zaidi ya kiafya ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki katika kipindi chote cha upapa wake wa miaka 12.
Maradhi ya Papa na hali yake mbaya ya kiafya vimeibua maswali kuhusu nani ataongoza Vatican na Kanisa Katoliki katika siku zijazo.
342/
