25 Februari 2025 - 17:27
"Ulaya ndiyo iliyopata hasara kubwa katika kamari ya Trump na Putin"

Wakati huu ambapo Saudi Arabia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano baina ya marais wa Russia na Marekani, kila kitu kinathibitisha kwamba aliyepata hasara kubwa katika kamari hiyo ni nchi za Ulaya.

Shirika la habari la FARS limeandika makala maalumu kuhusu suala hilo na sehemu moja ya makala hiyo inasema: "Macho yote yameelekezwa kwenye mkutano ujao kati ya marais wa Marekani na Russia huko mjini Riyadh, Saudi Arabia, lakini tarehe yake bado haijatajwa. Pamoja na hayo, kila kitu kinaonesha kuwa waliopata hasara kubwa katika kamari ya Donald Trump na Vladimir Putin, ni nchi za Ulaya."

Makamu wa Rais wa Russia, Yuri Ushakov amesema anaamini kuwa hakuna uwezekano wa kufanyika mkutano huo wiki ijayo. Amesema: "Kuna haja ya kutolewa fursa ya maandalizi zaidi kati ya wajumbe wa Marekani na Russia kabla ya kuainisha tarehe hasa ya mkutano huo."

Makala hiyo imeendelea kusema: "Inaonekana kwamba mkutano huo utafanyika baadaye mwezi huu, Kremlin imebainisha kuwa mkutano huo utafanyika hivi karibuni. Trump pia amesema kuwa muda wa mkutano huo uko karibu sana, lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu tarehe yenyewe hasa."

Mkutano huo umepangwa kufanyika baada ya mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya Marekani na Rusia yaliyofanyika mjini Riyadh Februari 18, 2025 na kudumu kwa saa nne.

Hayo yamekuja huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa limepasisha muswada wa kukomeshwa vita baina ya Russia na Ukraine. Naye Rais wa Ukraine, Vladimir Selensky amesema kwamba yuko tayari kujiuzulu. Azimio la kukomesha vita Ukraine limepasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bila ya kuwa na neno hata moja lililo dhidi ya Russia. Yote hayo ni udhibitisho kuwa, Ulaya ndiyo iliyokula hasara kwenye kamari hiyo.

342/