Amnesty International imeitaja hatua hiyo ya mgombea wa ukkansela wa Ujerumani na ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Sambamba na kumkosoa kiongozi huyo wa chama cha Christian Democratic Union, shirika hilo la haki za binadamu limesema katika taarifa yake kwamba:
Si mwanzo mzuri kama kansela mtarajiwa: Katika mkesha wa uchaguzi wa Bunge (Bundestag), Friedrich Merz anaonekana kumwalika Benjamin Netanyahu nchini Ujerumani, ambaye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imetoa hati ya kukamatwa kwake.
Sehemu nyingine ya taarifa ya Amnesty International imesema, hatua hii ni sawa na "wito wa wazi" wa kukiuka sheria na kusisitiza kwamba serikali mpya ya Ujerumani lazima iheshimu sheria za kimataifa na taasisi za haki za binadamu bila unafiki na undumakuwili.Mwezi Novemba mwaka jana (2024), Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa hati za kukamatwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na na aliyekuwa waziri wake wa vita Yoav Gallant baada ya kuwafungulia mashtaka ya kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu huko Gaza, ambako utawala wa Kizayuni uliendesha vita vya kinyama na kufanya mauaji ya kimbarii tangu mwezi wa Oktoba mwaka 2023.
342/
