3 Machi 2025 - 23:38
Source: Parstoday
Kiongozi Muadhamu: Iran inakabiliwa na muungano wa madola ya kinafiki

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Jamhuri ya Kiislamu haina tatizo na mataifa mengine; lakini hata hivyo inakabiliwa na muungano mpana wa "madola ya kinafiki" yanayojaribu kuingilia mambo yake ya ndani na kuvuruga uhusiano wake wa nje.

"Leo hii, wananchi wa Iran wanakabiliwa na mhimili mkubwa wa nguvu za kikafiri au za kinafiki," Ayatullah Ali Khamenei aliuambia mkusanyiko wa wasomaji na mahuffadh wa Qur'ani Tukufu jana Jumapili.

Mkutano huo wa Kiongozi Muadhamu na maqarii na mahuffadh wa Qur'ani Tukufu aghalabu hufanyika katika siku ya kwanza ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa, Iran haina matatizo na mataifa mengine na kuongeza kuwa, "Ni madola yenye mamlaka yanayoingilia mambo ya mataifa na nchi nyingine."

Ayatullah Khamenei pia ameashiria uwezo wa Qur'ani Tukufu katika kukabiliana na maradhi ya kijamii. Imam Khamenei amebainisiha kuwa, "Ikiwa Qur'ani itasomwa na kusikilizwa ipasavyo, maradhi yote yanaweza kutatuliwa." 

Kiongozi Muadhamu: Iran inakabiliwa na muungano wa madola ya kinafiki

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza bayana kuwa, Qur'ani haitoi tiba pekee bali pia mwongozo na motisha kwa waumini.

"Hili ni jambo muhimu. Wengi wanajua njia, lakini hawana motisha, na mifumo yao ya kiakili na kiadili inashindwa kuwatia moyo,” ameongeza Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha