Taarifa ya jumuiya hiyo ya Kiislamu imekosoa vikali hatua ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni ya kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imelaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kufunga vivuko vyote vya Ukanda wa Gaza.
OIC imesema hayo katika taarifa yake ya leo Jumatatu na kusisitiza kwamba, vitendo hivi haramu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu, Mkataba wa Geneva na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Aidha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu imeitaja hatua ya kuzingirwa Gaza kama aina ya adhabu ya pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ambayo, kwa mujibu wa Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, inahitaji kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa.
OIC imeitaka jamii ya kimataifa hususan Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni na kuhakikisha kutawala utulivu sambamba na misaada ya kibinadamu kupelekewa na kuingia Gaza bila ya vizuizi.
342/
Your Comment