Maandamano ya kupinga mpango huo yamekithiri na kushuhudiwa pia barani Ulaya.
Mara hii raia wa Sweden wamefanya maandamano ya kupinga mpango wa Rais wa Marekani wa kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina na siasa za Washington za kuunga mkono kikamilifu jinai za utawala wa Kizayuni.
Mamia ya watu walifanya maandamano katika mji wa Stockholm, mji mkuu wa Uswidi, kupinga mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuwatimua Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walipiga nara na kupaza sauti kupinga na kulaani mpango huo wa Trump ambao umeendelea kupingwa katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Tarehe 4 Februari, Donald Trump alitangaza, wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu huko Washington, kwamba nchi yake italitwaa eneo la Gaza baada ya kuwafukuza Wapalestina.
Rais Donald Trump wa Marekani amerudia mara kadhaa wito wake wa kulipora eneo la Gaza na kuwapatia makazi mengine Wapalestina wa eneo hilo ili kujenga kile alichokiita "Pwani ya Burudani ya Mashariki ya Kati". Wazo hilo limekataliwa na kupingwa vikali na Ulimwengu wa Kiarabu, pamoja na mataifa mengine mengi duniani, yakiutaja mpango huo wa Trump kuwa ni sawa na ufutaji wa kizazi.
342/
Your Comment